3 Septemba 2025 - 23:39
Source: Parstoday
Tehran yakadhibisha madai ya nchi za Kiarabu kuhusu visiwa vya Iran na kisima cha gesi cha Arash

Iran imesisitiza mamlaka iliyonayo kwa visiwa vitatu vilivyoko katika Ghuba ya Uajemi, haki yake kwa kisima cha gesi cha Arash na kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye malengo ya amani katika kujibu madai ya uongo katika taarifa ya hivi karibuni ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC).

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha madai yasiyo na msingi wa kisheria ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kuhusu visiwa vitatu vya Iran. Iran imebainisha haya katika taarifa yake ya jana. 

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi juzi Jumatatu walitoa taarifa katika mkutano wao wa pamoja na kudai kuwa visiwa vitatu kwa majina ya Tomb Kubwa, Tomb Ndogo na Bu Musa ni mali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imevitaja visiwa hivyo kuwa sehemu haiwezi kutenganishwa na ardhi ya Iran na kuongeza kuwa kukaririwa madai yasiyo na msingi katika taarifa zinazofanana hakutasababisha mabadiliko yoyote katika uhalisia wa kijiografia, kihistoria, na kisheria kuhusiana na visiwa hivyo.

Iran imesema itachukua hatua zozote zinazohitajika ili kuhakikisha usalama  wa visiwa vyake hivyo na kulinda maslahi ya nchi . 

Visiwa vitatu vya Bu Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo vinavyopatikana na Ghuba ya Uajemi kihistoria ni sehemu ya ardhi ya Iran; uthibitisho ambao unaweza kuthibitishwa na hati na nyaraka za nyingi za kihistoria, kisheria, na kijiografia nchini Iran na katika sehemu nyingine duniani. Hata hivyo, Umoja wa Falme za Kiarabu umekariri kutoa madai ya kumiliki visiwa hivyo. 

Your Comment

You are replying to: .
captcha